Marekani, Uingereza, Australia, Canada na New Zealand zimeilaumu China kwa kukiuka ahadi zake za kimataifa kwa uamuzi wa kufukuzwa kutoka bunge la Hong Kong wabunge wanaounga mkono demokrasia.
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa hayo matano washirika wamesema China inakwenda kinyume na ahadi yake ya mwaka wa 1984 kuwa itayaheshimu mamlaka ya ndani ya mji wa Hong Kong baada ya Uingereza kufikia uamuzi wa kukikabidhi kisiwa hicho kwa himaya ya China mwaka wa 1997.
Kuondolewa bungeni kwa wabunge wanne wa upinzani kulichochea kujiuzulu kwa wenzao wote wengine ikiwa ni hatua ya karibuni ya ukandamizaji unaoongezeka dhidi ya wakosoaji wa serikali ya China bara kwenye mji huo wenye mamlaka ya ndani.

No comments:
Post a Comment