Search This Blog

Friday, November 20, 2020

Chanjo za COVID-19 kuombewa kibali cha matumizi


Kampuni mbili za dawa za Pfizer na BioNtech zitawasilisha maombi ya kupatiwa kibali cha dharura kwa chanjo yake ya COVID-19 katika wakati Marekani inalenga kuanza kutoa chanjo hiyo baadae mwishoni mwa mwaka. 

Waziri wa afya wa Marakani Alex Azar amesema kampuni hizo zitaomba kibali cha muda kuanzia siku ya Ijumaa kutoka mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani iliyo na wajibu wa kutoa ruhusa ya aina hiyo. 

Ombi hilo pamoja na taarifa kutoka utafiti wa maabara uliofanywa kwa chanjo hiyo, vitapitiwa na jopo la wasayansi kabla ya kupatiwa ithibati. 

Kampuni hizo mbili zilitangaza mapema wiki hii kuwa chanjo waliyokuwa wakiifanyia utafiti imethibitisha kuwa uwezo wa kuzuia virusi vya corona kwa asilimia 95.

 Mafanikio kama hayo yalitangazwa pia na kampuni nyingine ya dawa nchini Marekani iitwayo Moderna ambayo hivi karibuni nayo itaanza mchakato wa kuomba kibali cha kutumika kwa chanjo waliyoitengeneza.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...