Serikali ya Ethiopia imetuma wahudumu afya kadhaa kutoka mji mkuu wa Addis Ababa kuelekea maeneo ya mpakani mwa mkoa wa Tigray ambako kuliendeshwa operesheni na chama cha waasi cha TPLF.
Utawala wa Addis Ababa ulitangaza kutuma baadhi ya madaktari na wahudumu wa afya kwenye eneo hilo kutoka hospitali na zahanati za mji mkuu.
Wakati huo huo, kampeni ya kukusanya damu kwa ajili ya wanajeshi na raia waliojeruhiwa pia inaarifiwa kuendelea.
Operesheni hiyo ya kijeshi inayoingia siku ya 13, imearifiwa kusababisha mamia ya watu kufariki na wengine kujeruhiwa hadi kufikia sasa.
Kwa mara ya mwisho, wakati jeshi la nchi likidhibiti kijiji cha Alamata mkoani Tigray, utawala wa Addis Ababa umekanusha taarifa zinazodai kuwa wanapanga kufanya mazungumzo na wajumbe wa TPLF kutoka Uganda.
Sudan imetangaza kuwa idadi ya wakimbizi walioingia nchini kutokana na mapigano ya kaskazini mwa Ethiopia inakaribia kufika 25,000.
TPLF ilitekeleza mashambulizi ya roketi katika mkoa wa Amhara na mji mkuu wa Asmara, Eritrea kwa madai ya serikali kuungwa mkono na jeshi.

No comments:
Post a Comment