Zaidi ya watu 700 wameripotiwa kutiwa mbaroni na vikosi vya usalama kwenye maandamano yaliyofanyika hapo jana kwa ajili ya kupinda serikali ya utawala nchini Belarus.
Msemaji kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Olga Chemodanova, alitoa maelezo kupitia mtandao wa kijamii na kuarifu kufanyika kwa maandamano kinyume cha sheria katika maeneo 35 kote nchini.
Chemodanova aliarifu kuwa maandamano hayo yameanza kupungua huku maafisa wa polisi wakichukua tahadhari zinazohitajika kuhakikisha hali ya utulivu na usalama inaimarika.
Akibainisha waandamanaji walionyesha hali ya kuzusha vurugu katika mji mkuu wa Minsk, Chemodanova alisema kuwa waandamanaji walifunga baadhi ya barabara na kuzuia magari na raia kupita.
Chemodanova aliongezea kusema kuwa waandamanaji hao walilazimika kukamatwa baada ya kukaidi agizo la kusitisha maandamano na tahadhari zilizotolewa na polisi.
Chemodanova pia alibainisha kuwa zaidi ya watu 250 walishiriki kwenye maandamano katika miji ya Brest na Grodno bila idhini, na kusema,
"Zaidi ya watu 700 waliokiuka sheria walikamatwa kwenye maandamano kote nchini na wataendelea kuwekwa chini ya ulinzi hadi watakapofikishwa mahakamani."
Baada ya Rais wa sasa Alexander Lukashenko kushinda uchaguzi wa urais uliofanyika Belarusi mnamo Agosti 9, maandamano yalianza dhidi yake kwa madai kwamba "uchaguzi haukutendeka kwa haki."
Waandamanaji wamekuwa wakiandamana kila wikendi nchini humo na kumtaka Rais Lukashenko aachie madaraka.

No comments:
Post a Comment