Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

Ujerumani yazituhumu Urusi na China kwa kutatiza vikwazo vya Korea Kaskazini


Ujerumani imezituhumu Urusi na China kwa kuizuwia kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa maamuzi ya endapo Korea Kaskazini imevunja marufuku ya Umoja wa Mataifa juu ya uingizaji wa mafuta ya petroli. 

Baraza hilo la Usalama limekuwa likiiwekea vikwazo Korea Kaskazini tangu mwaka 2006, katika jitihada za kuizuwia isiunde silaha za nyuklia na makombora ya masafa ya mbali. Mnamo mwaka 2017, liliiwekea nchi hiyo ya Asia ukomo wa matangi 500,000 ya mafuta kwa mwaka.

 Urusi na China ni mataifa pekee zinazopaswa kulijulisha Baraza la Usalama juu ya usafirishaji bidhaa za mafuta kwenda Korea Kaskazini, lakini zimekuwa zikifanya hivyo kwa kutaja tu kiwango cha tani na sio matangi ya mafuta. 

Kamati ya Baraza la Usalama hadi sasa imeshindwa kuamuwa endapo Korea Kaskazini imevunja vikwazo hivyo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...