Ethiopia imesema vikosi vyake vya kijeshi vinaelekea kwenye mji mkuu wa jimbo la Tigray baada ya vikosi vya waasi kukataa kujisalimisha na kuweka silaha zao chini, kufuatia wiki mbili za mapigano makali yaliyoitikisha nchi hiyona majirani zake wa Pembe ya Afrika.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed amesema kuwa sasa wanajeshi wake wanaingia kile alichokiita tukio la mwisho muhimu, akimaanisha kulichukuwa jimbo hilo la kaskazini kutoka mikononi mwa wapiganaji wa kundi la TPLF.
Jioni ya jana, kikosi maalum cha Abiy kwenye mzozo huo wa Tigray kiliwatuhumu waasi kwa kuyaharibu madaraja yanayouunganisha mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle, na maeneo mengine ya nchi, katika jitihada ya kuvizuwia vikosi vya serikali kuwafikia walipo.
Hadi sasa, Waziri Mkuu Abiy Ahmed amekataa miito ya mazungumzo kutoka jumuiya ya kimataifa akisema kuwa mazungumzo hayo yatafanyika tu baada ya kurejesha utawala wa sheria kwenye mkoa huo wa kaskazini.

No comments:
Post a Comment