Na Faruku Ngonyani,Mtwara
Kila ifikapo tarehe 17 Novemba kwa kila mwaka inakumbukwa siku ya Mtoto njiti duniani.
Siku hii kwa Mkoa wa Mtwara imeadhimishwa katika Hospitali ya Rufa ya Ligula kwa wataalamu wa afya kutoa elimu kwa akina mama wenye watoto njiti ili waweze kufahamu namna bora ya kuweza kuishinao watoto pindi wanapokuwa majumbani kwao.
Mkuu wa idara ya Watoto kutoka Hospitali hiyo ya Rufaa ya Ligula Dr.Hassani Katende amesema kuwa kutoka Januari mpaka Oktoba 2020 Hospitali hiyo ilipokea jumla ya watoto njiti 166 huku watoto 135 walikuwa wamevushwa.
Lakini pia Dr.Iren kutoka kitengo cha Watoto amewakumbusha akina mama hao juu ya changamoto anayokutananayo mtoto njiti pindi anapokuwa amezaliwa.
Ameelezea moja ya changamoto hizo ni pamoja na mtot njiti kushindwa namna ya kudhibi joto mwili hivyo amewashauri akina mama kuwaweka watoto wao kwenye vifua vyao ili waweze kupata joto la mama.
Lakini pia ameongeza kuwa kwa upande wa kunyenyesha na ni vyema mama akakamulia maziwa kwenye kikombe na kumnywesha mtot wake kwan mtoto njiti hana uwezo wa kuvuta maziwa kwa nguvu zake mwenyewe, na changamoto nyingine anayokutananayo Mtoto njiti ni pamoja suala zima la upumuaji ambapo mapafu yao hayana uwezo wa kusukuma hewa, hivyo basi Dr huyo amewashauri akina mama hao kutokuwaogesha watoto wao maji.
Nae Mganga Mfawidhi wa Hospatali ya Rufaa ya Ligula Dr.Albetina Mumlohowa ameongeza kuwa huduma ya utoaji kwa watoto awali ilikuwa changamoto kwa jamii ambapo walikuwa hawafahamua kama watoto njiti kama wanaweza kupona.
Na kwa sasa hamasa imeongezeka kwa jamii na wameweza kuwanusuru watoto Zaidi 130 kutoka mwezi Januri Mpaka Oktoba 2020

No comments:
Post a Comment