Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

Halmashauri ya vijiji Tarime kujenga vyoo kila soko kunusuru jamii na magonjwa ya mlipuko


Na Timothy Itembe Mara.

Halmashauri ya Tarime vijijini imejipanga kujenga vyoo kila soko na minada ili kuwanusuru wananchi wake na magonjwa ya mlipuko.

Akiongea na waandishi wa habari,Afisa Afya wa halmashauri hiyo,Mjaya Bwire Ofisini kwa mkuu wa wilaya Tarime,Ing Mtemi Msafiri,  alisema mradi huo utatekelezwa kupitia  mapato ya ndani.

Bwire alisema kuwa ili kuondokana na magonjwa ya mlipuko yanayosababisha rasilimali nyingi kupotea halmashauri yake imejipanga kujenga vyoo kila soko na minada kupitia mapato ya makusanyo ya ndani.

"Mradi huo wa ujenzi wa vyoo umeanza ndani ya vituo vyetu vya Afya na tutaenda mbali zaidi ambapo tumepanga kujenga vyoo katika masoko na minada ili kujenga jamii yenye Afya Bora na maendeleo endelevu"alisema Bwire.

Kwa upande wake Kaimu usafi wa mazingira wa halmashauri hiyo,Martha Mahule alisema kuwa halmashauri yake imejenga vyoo ndani ya vituo vya Afya zaidi ya 4 na ndani ya masoko na minada taklibani 6.

Mahule aliongeza kusema kuwa anatarajia kuona wananchi wanamwitikio wa kutoa ushirikiano na kupiga vita maradhi huku wa kizingatia  sheria na taratibu za mazingira na za kiavya.

Naye mkuu wa wilaya Tarime,Ing Mtemi Msafiri alisema usafi wa kitaifa wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi unaenda vizuri kwa wilaya Tarime na jamii inamwitikio mkubwa. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...