Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Jumla ya tani 3,230 na kilo 957 zimeuzwa na chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, kilichopo mkoani Lindi kupitia mnada wa sita kwa chama hicho na mnada wa 12 kwa mkoa wa Lindi, msimu wa 2020/2021.
Katika mnada huo uliofanyika leo mjini Nachingwe, bei ya juu ya korosho ghafi za daraja la kwanza ni shilingi 2,505 na bei ya chini shilingi 2,412 kila kilo moja.
Huku tani 30 za daraja la pili zikinunuliwa kwa shilingi 2,003 kila kilomoja. Katika ghala la Export ambalo lina tani 500 na kilo236 bei ya juu ni shilingi 2,488 na bei ya chini shilingi 2,484, ghala la Lindi farmers lenye tani 449 na kilo 489 bei ya juu ni shilingi 2,505 na bei ya chini 2,496.
Wakati ghala la Pachani lenye tani 640 na kilo 331 bei ya juu ni shilingi 2,488 na bei ya chini ni 2,488 kwani mnunuzi amenunua korosho zote zilizopo kwenye ghala hilo kwa bei hiyo.
Aidha katika ghala la Lipande lenye tani 550 na kilo 678 bei ya juu na chini ni shilingi 2,479. Kwani mnunuzi amenunua korosho zote zilizopo kwenye ghala hilo.
Wakati kwenye ghala la Umoja lenye tani 1,059 na 489 za daraja la kwanza bei ya juu ni shilingi Kwahiyo nidhahiri msimu utaendelea hata wakati wa kipindi cha mvua. Hivyo wakulima wanaweza kukusanya korosho zilizolowa na kupeleka moja kwa moja maghalani.
Alisema kitendo hicho kitasababisha kuharibu ubora wa zao hilo na kupunguza viwango vya bei sokoni.
Kwakuzingatia madhara ya kutodhibiti ubora, Mwaya amewaonya watendaji na viongozi wa AMCOS kwamba kitendo cha kupokea korosho zisizona ubora nikosa ambalo lina adhabu yake kwamujibu wa sheria.
Alibainisha kwamba watendaji na viongozi wasio zingatia miongozo na sheria watachukuliwa hatua za kisheria.
'' Kuna dalili za korosho kuendelea kuzaa hata katika kipindi cha mvua. Kwahiyo wakuli wanatakiwa kuwa waangalifu, waanike kwamuda usiopungua siku tatu ili kutunza ubora. Makambale yanaharibu soko, mwish o wa siku tutajikuta tunauza kwa bei zisizoridhisha,'' Mwaya alisisitiza.
Ofisa huyo wa CBT licha ya kuwaonya watendaji na viongozi hao wa AMCOS aliwaomba washiriki kikamilifu kuzuia korosho chafu zinazotoka nje ya mikoa ya Lindi na Mtwara zisiingie kwenye vyama vyao.
Kwani anataarifa kwamba kuna korosho chafu zinaingizwa katika mikoa hiyo.

No comments:
Post a Comment