Search This Blog

Sunday, November 15, 2020

Mkuu wa Mkoa Mbeya kukabidhi TRA majina 6 ya wakopeshaji wakwepa kodi

 


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema atakabidhi majina sita ya wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kujihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa wananchi kinyume cha utaratibu.


Chalamila amesema hao leo Novemba 15, 2020 wakati akizungumza na Mwananchi na kwamba amefuatilia na kujiridhisha na anao ushahidi wa kutosha.


"Nimejiridhisha kwa kufanya ufuatiliaji kwani wanakopesha mpaka mamilioni ya shilingi kwa wananchi na wanapokwama kulipa wanawanyanyasa kwa kushika mali zao," amesema.


Amesema akiwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa anahitaji TRA ifanye kazi yake kwa kuhakikisha wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa kuwa ni miongoni kwa wakwepa kodi na wahujumu uchumi.


Meneja wa TRA Mkoa, Eunice Liheruka amesema atafuatilia suala hilo na kuhakikisha wanabainika kwa kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria za nchi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...