Search This Blog

Sunday, November 15, 2020

Majaribio ya usafiri wa abiria wa mwendokasi wa juu zaidi

Usafiri wa kisasa wa abiria wa mwendokasi wa juu zaidi umefanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza katika jangwa la Nevada.


Usafiri huo unajumuisha vyumba ndani ya eneo la muundo wa tubu lisilo na kitu ulibeba wasafiri wawili kwa kasi ya juu mno.


Katika majaribio hayo - wafanyakazi wote wawili - walisafiri umbali wa mita 500 kwa sekunde 15 na kufikia umbali wa kilomita 172 kwa saa.


Hata hivyo kasi hiyo ni mfano tu wa kile kampuni hiyo inalenga kufikia yaani kasi ya zaidi ya kilomita 1,000 kwa saa.


Sio kwamba teknolojia hii ni ya kampuni ya Virgin Hyperloop pekee lakini hakuna kampuni ambayo imewahi kubeba abiria kwa kasi hiyo kabla.


Sara Luchian, mkurugenzi anayeshughulika na masuala ya wateja, alikuwa miongoni mwa wateja wawili na anaelezea safari hiyo kama ya "kusisimua kiakili na kimwili" amezungumza na BBC muda mfupi baada ya safari hiyo.


Yeye pamoja na afisa mkuu wa teknolojia Josh Giegel walivalia kawaida tu fulana na suruali za jeans badala ya suti maalum za kusafiri kama ilivyo kwenye anga.


Hatua hiyo ambayo imekuwa ikifanyiwa kazi kwa miaka kadhaa, imetokana na pendekezo la mwanzilishi wa kampuni hiyo Elon Musk. Baadhi ya wakosoaji wamekuwa wakiielezea kama sayansi ya kubuni.

Teknolojia hiyo imetokana na treni ya kasi zaidi duniani yenye kutumia sumaku kisha ikafanywa kuwa ya kasi zaidi kwa kutumia tubu zilizo na ombwe.


Treni zinazotumia sumaku ndio zilizorekodi kasi ya juu zaidi mwaka 2015 pale treni ya Japani ilipofanya majaribio na kufika umbali wa kilomita 601 kwa saa karibu na mlima Fuji.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...