Search This Blog

Tuesday, November 24, 2020

Manchester United yaitandika Instanbul Basaksehir bao 4-1

 


USIKU wa kuamkia leo Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Instanbul Basaksehir katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kulipa kisasi cha kufungwa mchezo wa kwanza

Watupiaji kwa Manchester United ni Bruno Fernandes alitupia mawili, dk ya 7 na 19, Marcus Rashford alitupia bao moja kwa penalti dakika ya 35 na msumari wa mwisho ni Daniel James dakika ya 90+2.

Lile la Instanbul Basaksehir ndani ya Uwanja wa Old Trafford lilipachikwa dakika ya 75 na Deniz Turuc ni kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Manchester United ikiwa kundi H ni vinara wakiwa na pointi 9 kibindoni na Insanbul ipo nafasi ya nne na pointi 3 ambazo ilizipata kwa Manchester United baada ya ushindi wa mabao 2-1,Novemba 11 Uwanja wa Basaksehir Fatih Terim.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...