Search This Blog

Friday, November 20, 2020

Hakimu ahukumiwa Miaka Mitatu kwa Rushwa

 


Na John Walter-Babati

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Isaka Kuppa amemhukumu kwenda jela miaka mitatu na kulipa faini  ya shilingi million moja na laki tano aliyekuwa hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo ya Magugu  Adeltus Richard Rweyendera.

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 13/11/2020 baada ya waendesha mashtaka wa takukuru  Martin Makami na Evelyne Onditi kuwasilisha ushahidi  dhidi ya mshitakiwa Rweyendera kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 1985 ambapo mahakama ilimkuta na hatia na kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  Holle Makungu alisema Rweyendera amepewa adhabu hiyo katika kesi ya rushwa namba CC .137/2020 baada ya kupatikana na hatia kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa  ya shilingi laki moja na nusu (150,000) kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya 11/2007.

Holle alieleza kuwa Rweyendera aliomba fedha hizo toka kwa wazazi wa ndugu wa washitakiwa  watatu ambao walikuwa wakishtakiwa kwenye kesi namba 242/2020ikiwa ni kishawishi cha kuwasaidia na kuwaachia huru wastakiwa hao kwenye kesi ambayo hakimu huyoalikuwa anaisikiliza katika mahakama ya mwanzo Magugu.

‘’Baada ya kupokea taarifa kutoka kw siri wetu ofisi yetu ilifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa ni kweli kesi hiyo ilikuwepo katika mahakama ya mwanzo ya magugu  na kwamba ilikuwa inasikilizwa na hakimu Adeltus Richard Rweyendera  ambapo uchunguzi wetu pia ulibaini watuhumiwa hao walikamatwa kwa tuhuma za uzururaji miongoni mwao wakiwa kwenye sehemu zao za biashara,kwa kuwa washitakiwa walikuwa watatu hakimu aliwataka wachangie elfu50 kila mmoja ambapo jumla ingekuwa laki moja na nusu”alisema Makungu.

Katika hatua nyingine takukuru Mkoani Manyara imewezesha askari wa wanyamapori Jumuiya tya hifadhi ya wanyamapori Burunge(JUHIBU)kulipwa stahiki zao zilizokuwa zimezuiliwa na spika wa jumuiya hiyo Ndg.Marcel Alfred Yeno.

Jumuiya ya Wanyamapori Burunge (WMA/JUHIBU) inajumuisha uhifadhi wa uhifadhi wa wanyamapori kwa lengo la kuinua hali ya kiuchumi na kustawisha maisha ya wanachama wake ambapo jumiya hiyo inaundwa na  vijiji 10vinavyozunguka hifadhi ya wanyama pori Tarangire.

Mkuu wa takukuru mkoani hapa alieleza uchunguzi uliofanywa na takukuru ulibaini juhibu iliingia mkataba wa kazi na kampuni ya Bouygues katika mradi wa umeme wa  400kv ambao unapita karibu na eneo la hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya tarangire kuelekea Namanga ambapo katika mkataba huo walikubaliana kila askari anayekwenda lindo alipwe shilingi elfu 25 kwa siku.

Alisema kati ya tarehe 27/7/2020  na 28/8/2020 askari 17 wa juhibu walishiriki katika ulinzi wa mradi huo wakitumia mishahara yao  huku wakiwa na matumaini kwamba wangelipwa  mwisho wa mwezi stahiki zao kwa mujibu wa mkaba lakini hawakulipwa.

Uchunguzi umebaini kuwa kampuni ya Bouygues walilipa kiasi cha million 2 na laki 3 kwenye akaunti ya juhibu kwa ajili ya skari hao lakini spika huyo akadhuiya kuidhinisha malipo hayo na kuwalazimisha askari hao kutia sahihi karatasi za malipo ili kuonyesha kuwa wamelipwa na kudai kwamba wale ambao wangekataa angewapeleka kwenye kazi cha kuwaazimia kufukuzwa kazi.

Makungu alisema kitendo hicho kilichofanywa na spika  Marcel ni matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha sheria cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya 2007  hivyo baada ya takukuru kuingilia kati kwa askari kulipwa haki zao pia wamemtaka spika huyo ajipime iwapo anastahili kuendelea kuiongoza juhibu kabla hajachukuliwa hatua.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...