Search This Blog

Tuesday, October 6, 2020

WHO: Chanjo ya Covid-19 inaweza kupatikana mwishoni mwa mwaka huu



Chanjo ya virusi vya corona inaweza kupatikana mwishoni mwa mwaka huu, kwa mujibu wa mkuu wa shirika la afya duniani WHO. Mkurungenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametoa wito wa mshikamano na dhamira ya kisiasa kwa viongozi wote, ili kuhakikisha kwamba chanjo zitatolewa kwa usawa. 

“Tunahitaji chanjo, na kuna matumaini kwamba mwishoni mwa mwaka tunaweza kupata chanjo. Hakika kuna matumaini," amesema Tedros, katika hotuba ya kufunga kikao cha bodi cha uongozi wa WHO. Chanjo tisa za majiribio ziko kwenye ratiba ya kituo cha chanjo cha kimataifa cha WHO, COVAX, ambacho kinakusudia kusambaza dozi billioni 2 kufikia mwisho mwa 2021. 

Mkutano huo wa siku mbili wa bodi ya uongozi wa WHO, ulichunguza namna ulimwengu unavyopambana, na janga la Covid-19, na ulisikia wito kutoka Ujerumani, Uingereza na Austria, kuhusu kuimarisha shirika hilo la umoja wa mataifa. Utawala wa rais wa Marekani, Donald Trump, uliikosoa WHO namna inavyoshughulikia janga hili. 


Pia umeshutumu WHO, kushirikiana na China, na haikutekeleza jukumu lake kwa kuiwajibisha juu ya vitendo vyake, wakati virusi vya corona vilipoanza kwa mara ya kwanza mwaka uliopita. 


Lakini Tredros alitupilia mbali madai hayo ya Marekani, na kusema kwamba WHO, iliendelea kutoa taarifa kwa ulimwengu.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...