Search This Blog

Tuesday, October 6, 2020

Zitto Kabwe apata ajali mkoani Kigoma



Chama cha ACT-Wazalendi kimeeleza kuwa kiongozi wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini


Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari iliyotolewa na Afisa Habari ACT-Wazalendo, Arodia Peter, ilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana ambapo Zitto alikuwa na watu watano kwenye gari yake.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo Zitto na watu hao ote wako salama ingawa walipata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba baada ya ajali hiyo walipata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye walipelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...