Search This Blog

Saturday, October 24, 2020

Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuongoza nchi



NA THABIT MADAI, ZANZIBAR

WAANACHI wa Zanzibar wametakiwa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuongoza nchi na sio kuchagua viongozi wanao wahamasisha kuvunjifu wa amani iliyopo Oktoba 27.

Katibu wa Umoja wa Vyama vya siasa, Ameir Hassan Ameir, aliyasema hayo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Kikwajuni Mjini Unguja.

Alisema, kumekuwepo kwa baadhi ya anasiasa wasioitakia mema nchi ya Zanzibar ambao wakuwa wakiwahamasisha wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura Oktoba 27 jambo ambalo linaashiria kuleta machafuko katika nchi.

Alisema, Oktoba 27 itakuwa ni watu maalum ambao wamewekwa kisheria kwa mujibu wa muongozo wa tume ya uchaguzi na Oktoba 28 itakuwa ni siku ya wananchi wote waliokuwa wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Aidha alisema kuwa, wanasiasa hao wamekuwa na dhamira ovu ya kutaka kuharibu uchaguzi na kutoitakia mema nchi ya Zanzibar.

Nae, mgombea Urais kupitia chama cha UPDP,  Hamad Mohammed Ibrahim,  alisema kuwa viongozi wa Vyama hivyo, wamekuwa na lengo la kurudisha fadhila kwa wafadhili wao kwani wamekuwa wakifadhiliwa kila baada ya uchaguzi kukaribia.

Aidha alisema kuwa, ni vyema wanasiasa hao, kuwapuuza kwani wamekuwa na dhamira ovu ya kuleta machafuko na kuwataka wajitokeze tarehe 28 ili kuweza kumchagua kiongozi atakayeweza kuiongoza Zanzibar.

Sambamba na hayo, alisema kuwa Zanzibar, itaendelea kujengwa na Wazanzibar wenyewe na wananchi wasihamasike kufanya vurugu na  isitokee fursa ya kuvunja udugu uliokuwepo.

Nae,  Peter Agathon Magwira kutoka DP, aliwahimiza wananchi wa Zanzibar kuendelea kuitunza amani iliyopo na kuwataka watakapomaliza kupiga kura ifikapo Oktoba 28 warudi majumbani kusikiliza matokeo ya uchaguzi.

Aidha aliviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukukia hatua stahiki viongozi wanaojaribu kuchafua amani iliyopo ambapo wamekuwa akitoamatamko kwenye majukwaa yao ya kisiasa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...