NA THABIT MADAI
MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema, kuwa anatafumbua kuwa Mabalozi ndio nguzo ya Chama hicho, hivyo ataendelea kuwatambua na kuwathamini katika chama hivyo aliwataka wahamasishane kwenda kupiga kura wakati ukifika.
Amesema kuwa muda wote Chama cha CCM kimefanya kampeni za kisasa na kistarabu kwa kuwaomba wananchi ridhaa ya kwenda kukipatia ushindi mkubwa Chama cha CCM ifikapo Oktoba 28.
Aliyasema hayo, alipokuwa akizungumza na Mabalozi wa Mkoa wa Magharibi Kichama kikao ambacho limefanyika katika ukumbi wa CCM Amani.
Alisema kuwa Mabalozi watapewa mstari wa mbele kwa kuwezeshwa ili ushindi upatikane na waweze kuwatoa watu wao kwa kwenda kupigakura.
Aidha alisema kuwa katika serikali hiyo, atahakikisha ataendeleza yote yaliyoachwa na serikali ya awamu ya saba kwa kuanzia.
Akizungumzia uzembe serikali, alisema kuwa ataunda serikali itakayotekeleza majukumu yao kwa watu kuwa kuwafanya wawwajibike kiutendaji katika serikali yake.
Alisema kuwa matumaini makubwa ninkuletamaendeleo katika serikali yake.
Alisema kuwa Mabalozi wamempa matumaninmakubwa yakiwa wanamsapoti katika serikali atakayoiunda.
Alisema kuwa ataunda serikali na siku ya kuapishwa Mabalozi wote wataalikwa katika kuapishwa kwake.
Sambamba hayo, aliwataka wanawake navijana kuendeleza ari yao ya kuengezakura wakati ukifika na kutofanyamakosa
"Mukinichagua Mimi kura rais wa Zanzibar kutaandika history kuwa nitakuwa rais wa kwanza niliyozaiwa baada ya Mapinduzi"
Hivyo, aliahidi kuendelea kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi yaliyofanyika 1964 pamoja na kuulinda Muungano ulioasisiwa na wazee wa Taifa hili.
"Dhamira yangu ni kuwatumikia wazanzibar na sina shaka na mungu ataniwezesha na sina budi tutasinda na kutaendeleza maendeleo katika nchi yetu" alisema.
Akitoa salam za Mabalozi wa Mkoa wa Magharibi Kichama, Salama, alimuhakikishia mgombea huyo wakati ukifika watahamasisha nyumba zao kutoka kwenda kupiga kura ili kumpigia mgombea huyo ili ushindi upatikane mkubwa.
Aidha alisema kuwa mabalozi wa Mkoa huo wanafahamu utendaji wa kazi wa Dk. Mwinyi, hivyo, hawana budi kumpigia kura ifikapo Oktoba 28 ili aweze kuwa rais wa Zanzibar.
"Tunahakikisha kuwa sisi mabalozi tunawahamasisha wananchi wetu kutoka mapema kwenda kupiga kura ili ushindi upatikane mapema" alisema.
Sambamba hayo, walimtaka mgombea huyo, endapo ataingia madarakani kuhakikisha anawachukulia hatua stahili watendaji wazembe katika serikali ili kuweza kuipa heshima serikali yake.
Alisema kuwa hali ya kisasa, katika Mkoa huo, kwa sasa unaendelea vizuri na hakuna vitisho vya aina yoyote vilivyojitokeza katika Mkoa huo.
Sambamba na hayo, alimpongeza uongozi wa serikali ya awamu ya saba iliyoongozwa na Dk. Ali Mohmed Shein, kwani imeweza kutekelleza huduma muhimu katika mitaa mbalimbali ikiwemo vituo vya afya, elimu na huduma ya maji Safi na salama.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Magharibi Kichama, Mgeni Mussa Haji,alisema, kuwa Mabalozi wapo tayari kuwatoa wapiga kura katika nyumba zao ili waende wakatekeleze haki yao ya msingi ya kupigakura.

No comments:
Post a Comment