Watawala wa kijeshi nchini Mali wameahirisha mkutano wao wa kwanza uliohusu mpango wa kurejesha madaraka kwa raia baada ya kuongezeka kwa mvutano miongoni mwa viongozi wakuu ambao walisababisha mapinduzi ya Agosti 18.
Wanajeshi waliyaalika makundi ya asasi za kiraia, vyama vya siasa na waasi wa zamani kwa lengo la kufanikisha mashauriano.
Lakini taarifa ya watawala hao wa kijeshi ilieleza kwamba mkutano umeahirishwa katika dakika za mwisho hapo jana hadi utakapotajwa tena kutokana na kile walichosema "sababu za kimaandalizi".
Kundi la muungano wa waandamanaji ambalo lilikuwa likifanya maandamano dhidi ya rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keita, linalojulikana kama "June 5 Movement" halikualikwa kushiriki mkutano huo.
Kundi hilo linataka utawala wa kijeshi kuwajibika katika kufanikisha utawala wa kiraia kama ulivyoahidi, pamoja na kutoainishwa muda.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment