Maelfu ya Waisrael wamefanya maandamano hapo jana mjini Jerusalem, ikiwa ni muendelezo wa mikusanyiko ya kila mwishoni mwa juma katika kipindi hiki cha kiangazi, yenye lengo la kushinikiza kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambae anakabiliwa na kesi ya rushwa na kushindwa kulishughulikia vyema janga la virusi vya corona.
Maandamano mengine madogo, madogo yalifanyika pia katika maeneo mengine ya Israel, likiwemo la mji wa Caesaria, ambako kuna makazi binafsi ya Netanyahu.
Katika mkusanyiko mkubwa mjini Jerusalem, waandamanaji walikusanyika katika eneo la kuingilia mji huo na katika makazi rasmi ya Netanyahu, wakiwa wameshika bendera ya Israel na nyingine nyeusi ikiwa ni ishara ya moja ya harakati za kupinga.
Serikali ya muungano ya Israel hivi karibuni ilinusurika kuvunjika baada ya kushindwa kufikia makubaliano kuhusu bajeti.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment