Treni hiyo ya mizigo imefanya safari hiyo ya majaribio ikitokea jijini Tanga baada ya kukamilika kwa ufufuaji wa kipande cha reli cha kuutoka Moshi hadi Arusha chenye urefu wa kilometa 86.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenani Kihongozi na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro wamewaongoza wananchi wa mkoa wa Arusha kuipokea treni hiyo ambapo wameeleza kufufuliwa kwa usafiri wa reli kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.
Kwa upande wao wananchi wa mkoa wa Arusha James Peter Ndarivoi na Aisha Mbaraka wameeleza kuwa usafiri huo kutaokoa muda wanaopoteza kwenda kuchukuwa bidhaa Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Nchini,TRC Focus Makoye ameeleza kuwa sasa wanatarajia kuanza rasmi safari za treni ya abiria pamoja na ya mizigo.
Ufufuaji wa Reli hiyo kati ya Korogwe hadi Arusha umegharibu shilingi bilioni 14 ambapo sasa usafiri wa gari Moshi utaunganisha kati ya Dar-es Salaam na Arusha katika umbali wa kilometa 644 huku nauli ya chini ikiwa shilingi 18,000.

No comments:
Post a Comment