Machibya amesomewa mashtaka yake leo 10/08/2020 na Wakili Mwandamizi wa Jamhuri, Simon Wankyo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya
Mbali na shtaka la kusimamia biashara hiyo haramu ya Upatu, Mr. Kuku anayekabilia na Kesi ya Uhujumu Uchumi pia ana mashtaka ya Kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa Umma bila leseni na kutakatisha fedha
Anatuhumiwa kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa Umma akiwadanganya kuwa watafanya Ujasiriamali wa ufugaji wa kuku na watapata faida ya asilimia 70 kwa waliowekeza kwa miezi 8 na asilimia 90 kwa waliowekeza kwa miezi 6, kiasi kinachoelezwa kuwa kikubwa kuliko mtaji uliokusanywa
Pia, kati ya Aprili 26, 2019 na Januari 26, 2020 jijini Dar anadaiwa kujihusisha na miamala ya Tsh. Bilioni 6.4 kutoa katika akaunti iliyoitwa Mr. Kuku Pharmacy katika Benki ya CRDB huku akijua fedha hizo ni zao tangulizi la biashara haramu ya Upatu
Aidha, anadaiwa kupokea fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 17 ya maingizo ya Umma bila kuwa na leseni. Upande wa Mashtaka umesema upelelezi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Agosti 24, 2020 huku mtuhumiwa akirudi rumande kutokana na makosa hayo kutokuwa na dhamana
No comments:
Post a Comment