Search This Blog

Wednesday, July 22, 2020

Wakulima zaidi ya mia nne kulipwa fedha zao za Korosho Mkoani Mtwara


Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Wakulima Zaidi ya Mia Nne (400) wa zao la korosho waliokuwa wadai fedha zao  kwa msimu wa 2019/2020 Mkoani Mtwara kulipwa ndani ya wiki hii.

Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa benki ya Maendelendeo  ya Kilimo Tanzania Japhet Justin  alipokuwa anazungumza na wakuu wa idara za Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani Pamoja na Halmashuri ya Wilaya ya Mtwara.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa Mkoa wa Mtwara wakulima wanadai bilioni 12 huku Wilaya ya Tandahimba kuna deni la bilioni 9,Wilaya ya Mtwara Milioni 844 na Wilaya ya masasi bilioni mbili (2).

Awali  madeni ya wakulima kwa Mkoa mzima wa Mtwara yalikuwa  Bilioni Mia nne na Moja (401) .

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ameeleza mpaka kufika siku ya Juma mosi tarehe 25 julai 2020 wakulima kwa kiasi kikubwa watakuwa wamepata fedha zao:  ”haya madeni yote yanakwenda kuondoka na nina uhakika hizi siku zinavyozidi kwenda mpaka kufikia juma mosi mpaka ya  ijayo haya madeni yote yatakuwa yamelipwa”

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...