Search This Blog

Wednesday, July 22, 2020

Makamanda na wanamgambo 45 wa Taliban wauawa katika shambulio la anga la jeshi la Afghanistan


Wanachama wasiopungua 45 wa kundi la Taliban wakiwemo makamanda na wanamgambo wa kundi hilo wameuawa katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi la Afghanistan katika wilaya ya Adraskan jimboni Herat magharibi mwa nchi hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Adraskan ametangaza kuwa, wanachama 45 wa kundi la Taliban wameuawa na wengine 16 wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililolenga eneo walipokuwa wamekusanyika watu hao.
Msemaji wa Gavana wa jimbo la Herat, Gilani Farhad amesema, makamanda hao wa kundi la Taliban pamoja na wanamgambo wao walishambuliwa wakiwa wanaandaa na kuratibu mashambulio ya kigaidi.
Wakati huohuo, askari wa serikali ya Afghanistan wamewatia nguvuni wanachama wanne wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) katika jimbo la Nangarhar mashariki mwa nchi hiyo.

Kwengineko nchini Afghanistan, watu wenye silaha wasiojulikana, jana Jumatano waliwapiga risasi na kuwaua askari watatu wa usalama barabarani katika jimbo la Samangan kaskazini mwa nchi.
Hayo yanajiri huku miito ikiendelea kutolewa kulitaka kundi la Taliban lijiunge na mchakato wa kutafuta suluhu na kurejesha amani nchini Afghanistan


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...