Search This Blog

Wednesday, July 22, 2020

Bunge laahirishwa Zambia baada ya mbunge kufariki na corona


Bunge la Zambia limelazimika kufungwa baada ya Msajili wa Bunge, Rogers Mwewa kufariki baada ya kupata maambukizi ya Corona Virus

Mwewa alifariki na kuzikwa Julai 21. Makamu wa Rais, Inonge Wina amesema kutokana na kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya #COVID19 wamelazimika kuahirisha Bunge

Spika wa Bunge la Zambia, Patrick Matibini ataongoza katika zoezi la upimaji wa Corona Virus kwa Wabunge wote na zoezi linatarajiwa kufanyika katika kliniki ya Bunge, Lusaka

Karani wa Bunge, Cecilia Mbewe amesema hadi kufikia Julai 15, Wabunge 3 wamekutwa na COVID19, pia wafanyakazi 10 wa Bunge wamekutwa na maambukizi pamoja na wengine 6 ambao sio wafanyakazi wa Bungeni



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...