Search This Blog

Wednesday, July 29, 2020

Tetesi za soka za Kimataifa

Kocha wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho anataka kumsajili winga anayekipiga Porto, raia wa Colombia Luis Diaz, 23.

Inter Miami, inayomilikiwa na nahodha wa zamani wa England David Beckham, ina mpango wa kumfanya mshambuliaji wa Barcelona Luiz Suarez kuwa chaguo lao la kwanza kubwa la usajili (Mundo Deportivo - in Spanish)

Wakala wa mchezaji David Alaba, wametaka Bayern Munich kumlipa pauni milioni 18

Wakala wa mchezaji anayetolewa macho na Manchester City na Paris St-Germain David Alaba, ameitaka Bayern Munich kumlipa mchezaji beki huyo wa kushoto, 28, pauni milioni 18 kuongeza mkataba wake (Bild)

Mazungumzo kati ya Manchester United na mlinda mlango wa Kiingereza Dean Henderson, 23- ambaye ametumia msimu wake akichezea Sheffield United kwa mkopo- yamekuwa kwenye hatua muhimu baada ya kufanyika kwa majuma kadhaa (Sky Sports)

Atletico Madrid imekataa ofa ya pauni milioni 22.6, na kiungo wa kati Matteo Guendouzi, kutoka Arsenal kwa ajili ya kiungo wa kati Thomas Partey, 27 (AS in Spanish)

Chelsea imeweka kipaumbele katika kumsajili beki wa kushoto wa Leicester City Ben Chilwell, 23, miongoni mwa machaguo mengine ya nafasi hiyo, akiwemo mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Ajax Muajentina Nicholas Tagliafico,27.(Goal)

Watford iko kwenye mazungumzo na Vladimir Ivic kuhusu nafasi ya kocha iliyo wazi baada ya Mserbia huyo, 43 kuondoka Maccabi Tel Aviv, ambako alinyakua mataji kadhaa ya ligi, mfululizo. (Mail)

Mshambuliaji Mbrazili Hulk, 34, anafikiria kuhamia ligi ya primia mkataba wake na Shanghai SIPG utakapokwisha mwezi Januari. (Talksport)

Hatahivyo matumaini ya Leeds ya kumsajili winga Thiago Almada yanafifia, huku mchezaji huyo, 19 akiwaambia wachezaji wenzake wa timu ya Velez Sarsfield kuwa anataka kubaki katika ardhi ya nyumbani kwake (Leeds Live)

Mlinda mlango wa zamani wa Burnely, West Ham na Manchester City Joe Hart, karibuni kujiunga na mabingwa wa ligi ya Uskoti, Celtic. (Sun)

Barcelona wanatarajia kumuuza Martin Braithwaite, 29. Mshambuliaji huyo si mchezaji aliye kwenye mipango ya kocha Quique Setien msimu ujao. (Mundo Deportiv )


Leeds United wanaandaa kitita cha pauni milioni 15 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Tottenham, Muajentina Juna Foyth, 22. (Sun)

Roma bado haijafikia makubaliano na Manchester United kuhusu kumsajili kwa mkataba wa kudumu mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Chris Smalling, 30. (Corriere dello Sport-in Italian)

Lazio wako kwenye mazungumzo kumsajili kiungo mchezeshaji wa Manchester City David Silva, 34. (AS)

Kiungo wa Chelsea Willian, 31, ambaye anamaliza mkataba wake msimu huu, ana ''ofa mbili'' kutoka kwenye vilabu vya primia, amesema wakala wake. (Talksport)

Everton wanataka kumsajili mchezaji wa zamani wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic

Everton wanataka kumsajili mchezaji wa zamani wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic, 36, kutoka Zenit Saint Petersburg. (Vecernjih Novosti-in Serbian)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mbelgiji Jan Vertonghen, 33, amesema analo chaguo kuhusu wapi anakotaka kuelekea baada ya kuondoka Tottenham (Talksport)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...