Search This Blog
Monday, July 13, 2020
Merkel:Huenda Umoja wa Ulaya usikubaliane kuhusu ufufuaji uchumi
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema jana Jumatatu kwamba bado haijulikani ikiwa viongozi wa Umoja wa Ulaya watakubaliana wakati wa mkutano wao wa kilele wiki hii kuhusu mfuko wa euro bilioni 750 wa kupiga jeki uchumi ambao umeathiriwa na janga la corona, mnamo wakati kuna pingamizi kutoka kwa baadhi ya nchi.
Akizungumza baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte karibu na mji wa Berlin, Merkel amesema bado kuna changamoto ya muafaka, lakini amesisitiza kwamba mfuko huo wa kufufua chumi, unapaswa kuwa wa kitita kikubwa na si kupunguzwa, kwa sababu kazi iliyoko ni kubwa.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa kwa mkutano maalum wa kilele wa umoja huo utakaofanyika Ijumaa kuujadili mfuko huo. Giuseppe Conte ametaka makubaliano kupatikana haraka huku akionya kwamba mkwamo utasababisha athari kubwa kwa uchumi wa Umoja wa Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment