Search This Blog

Monday, July 13, 2020

Mkuu wa jeshi la Somalia anusurika kifo, raia mmoja auawa katika shambulizi la al Shabab




Msemaji wa jeshi la Somalia Kanali Abdiqani Ali amesema kuwa, Jenerali Yusuf Rage alikuwa akiendesha gari katika msafara wa jeshi karibu na hospitali moja ya kijeshi kwenye wilaya ya Hondan ya mkoa wa Mogadishu wakati wa shambulio hilo.
Kanali Abdiqani Ali ameongeza kuwa walinzi wa Jenerali Rage walilifyatulia risasi gari lililokuwa limesheheni mabomu lililokuwa likijaribu kugonga msafara huo na kwamba gaidi aliyekuwemo ameuawa na gari limeripuka. Ameongeza kuwa, shambulizi hilo limeua raia mmoja na kwamba mkuu wa jeshi la Somalia na walinzi wake hawakupatwa na madhara ya aina yoyote.
Msemaji wa operesheni za kijeshi za kundi la al Shabab, Abdiasis Abu Musab ametoa taarifa akisema, kundi hilo ndilo lililopanga na kutekeleza shambulizi hilo la kujitoa mhanga mjini Mogadishu.



Kundi la al Shabab limekuwa likifanya mashambulizi ya kigaidi nchini Somalia tangu mwaka 2008 kwa shabaha eti ya kusisi utawa wa Kiislamu.
Kundi hilo linapigwa vita na wasomi wa Kiislamu wanaosema linafuata itikadi zisizo sahihi za kundi la Kiwahabi linalofasiri isivyo mafundisho na sheria za Uislamu.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...