Search This Blog

Monday, July 13, 2020

Pompeo: Madai ya China katika bahari ya Kusini mwa China ni kinyume cha sheria


Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo, amesema Marekani itachukulia juhudi za China kutaka kudhibiti rasilmali katika bahari inayozozaniwa ya kusini mwa China kuwa kinyume cha sheria, hatua ambayo huenda ikawa mzozo mwingine kati ya nchi hizo.

Marekani ilishayapinga madai ya China kuhusu bahari iliyoko kusini mwa China, na badala yake kukubaliana na Vietnam, Ufilipino pamoja na washirika wake wengine katika kanda hiyo.

Kwenye taarifa, Pompeo pia aliyapinga madai ya China kuhusu umiliki wa kisiwa kinachozozaniwa cha Spratly, ambacho mapema mwaka huu, China ilitangaza kuwa ni wilaya inayoisimamia, hali ambayo itaiwezesha kutanua mipaka yake baharini.

Taarifa hiyo ya Marekani ndiyo hatua ya hivi karibuni ya utawala wa Rais Donald Trump dhidi ya China. Katika wiki za hivi karibuni, Rais Trump aliwawekea vizuizi maafisa wa China kuhusiana na madai ya ukiukaji wa haki dhidi ya jamii ya Uighur na Tibeta.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...