Search This Blog
Sunday, July 5, 2020
Marekani iliwapa magaidi zawadi kubwa zaidi kwa kumuua kigaidi Luteni Jenerali Soleimani
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuuawa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda shahidi wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ilikuwa ni zawadi kubwa zaidi ya Marekani kwa magaidi wakufurishaji na waungaji mkono wao.
Itakumbukwa kuwa shahidi Qassem Soleimani, na Abu Mahdi al-Muhandis Naibu Kamanda wa Kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, Al Hashd Al Shaabi, waliuawa wakiwa na wenzao wengine wanane tarehe tatu Januari mwaka huu, katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa na askari magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Baghdad, Iraq. Shahidi Soleimani alikuwa nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo.
Akizungumza Jumamosi mjini Tehran katika kikao cha kufutilia kisiasa na kisheria kadhia ya kuuawa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani na wenzake, Admeri Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amekumbusha kuwa: "Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel zilikuwa na chuki dhidi ya Shahidi Soleimani na Shahidi al Muhandis kwa sababu wawili hao walikuwa na nafasi muhimu na ya kipekee katika vita dhidi ya magaidi wakufurishaji katika eneo na hivyo waliweza kufichua namna ambavyo Marekani ilikuwa inauhadaa ulimwengu kwa kudai kuwa inapambana na ugaidi."
Shamkhani ameendelea kusema kuwa, walimwengu wanapaswa kuwashukuru viongozi halisi wanaojitolea kupigana vita dhidi ya ugaidi. Amesema uongozi shupavu wa kijeshi na jitihada zilizojaa ikhlasi za Shahidi Soleimani na Shahidi Al Muhandis ndio sababu ya kuzuia kuenea zaidi fitina ya magaidi wakufurishaji kote duniani. Katika kikao hicho, maafisa wa vitengo vya kisheria, kisiasa, kiusalama na kijeshi nchini Iran wamejadili njia za kufuatilia kadhia ya kuuawa shahidi makamanda wa muqawama.
Wiki iliyopita, Mwendesha Mashtaka wa Tehran alitoa waranti wa kutiwa mbaroni watu 36 akiwemo Rais Donald Trump wa Marekani wakihusishwa na mauaji ya Shahid Qassem Soleimani.
Mwendesha Mashtaka wa Tehran alieleza kuwa, tayari wameitaka Polisi ya Kimataifa Interpol kuwatia mbaroni wahalifu hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment