Search This Blog

Tuesday, July 21, 2020

"Malipo ni duniani, mwisho wa ubaya aibu" - Prof J


Msanii na Mbunge anayeoongoza watu na wanyama Jimbo la Mikumi Prof Jay, amesema kuwa kwenye maisha haya amejifunza kuchunga sana mdomo wake kwa sababu malipo ni hapa hapa duniani na mwisho wa ubaya ni aibu.


Akitoa funzo hilo kupitia post aliyoweka kwenye mtandao wa Instagram na Twitter Prof Jay ameandika kuwa, "Nimejifunza kwamba sisi wanadamu inatupasa kuchunga sana ndimi zetu, kutafakari kwa kina kauli zetu na inapobidi ni kufunga kabisa mabakuli yetu kwani malipo yapo hapa hapa duniani na mwisho wa ubaya ni aibu"  kutoka kwa Prof Jay.
Tayari Prof Jay ametangaza nia ya kugombania tena kwa miaka mitano ijayo ya kuwatumikia wananchi wake wa Jimbo la Mikumi, Mkoani Morogoro.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...