Search This Blog

Tuesday, July 21, 2020

Trump akubali janga la corona 'litaathiri vibaya' kabla ya hali kuimarika


Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini humo huenda ukawa "mbaya zaid kabla ya hali kuimarika", wakati alipofufua tena mazungumzo yake na wanahabari.

Bw. Trump pia ametoa wito kwa Wamarekani wote kuvalia barakoa, akisema kuwa "zitasaidia kudhibiti maambukizi" na kwamba ni ishara ya "uzalendo".

Rais, hakua amevalia barakoa wakati akitoa maelezo kwa wanahabari, lakini aliwahi kupuuza suala la kuvaa kifaa kinga hicho.

Inasemekana wasaidizi wake wamemuasa kuchukua hatua zenye malengo wakati ambapo maambukizi yanazidi kuongezeka kote Marekani.

Utoaji taarifa kuhusu corona kwa vyombo vya habari kutoka Ikulu ya Marekani, mwisho ilikuwa Aprili punde tu baada ya Trump kusema kuwa virusi hivyo vinaweza kutibiwa kwa watu kujipaka dawa za kuua vijidudu.

Baada ya miezi kadhaa, taarifa yake ya Jumanne ambayo ilionekana kupangwa, rais aliashiria kuunga mkono kile ambacho maafisa wa afya wamekuwa wakisema kupitia jopo lake la kukabiliana na ugonjwa huo na kuonya kwamba: "Kwa bahati mbaya hali huenda ikawa mbaya zaidi kabla ya kuanza kubadilika.

"Wakati mwingine huenda sipendi kusema kuhusu mambo, lakini hivyo ndivyo ilivyo."

Aliongeza: "Tunataka kila mmoja ikiwa atashindwa kutekeleza kanuni ya kutokaribiana, avae barakoa.

"Ama uwe unapenda barakoa au la, zina machango wake, zitakuwa na athari yake na tunahitaji kila kitu tunachoweza kupata."

Bwana Trump - ambaye zaidi ya mara moja alirejelea kuwa ugonjwa wa Covid-19 ni "virusi vya China" - akiwa anatoa taarifa hiyo, alitoa barakoa mfukoni kwake, lakini hakuivaa.

Rais huyo ana kibarua kigumu wakati anapotafuta kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi wa urais Novemba dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Democratic, Joe Biden, kulingana na kura za maoni.

Bwana Biden Jumanne alimshutumu Bwana Trump kwa kushindwa kukabiliana na janga la virusi vya corona. "Amewaondokea nyinyi, ametenga nchi hii," aliyekuwa makamu rais wa Marekani alisema.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...