Search This Blog

Thursday, July 16, 2020

Lulu afunguka kinachokwamisha ndoa yake

Staa wa Filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amesema kuwa aharakishi kuingia kwenye ndoa kutokana bado kuna vitu anahitaji kufanya yeye kama msanii, hivyo atakapoingia kwenye ndoa hataweza kutekeleza hayo vizuri.

Lulu ameeleza hayo jana pale alipodakwa na wanahabari akitokea katika hafla ya uhamishaji wa COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda kwenda Wizara ya Habari ili kuziweka pamoja mamlaka zinazosimamia wasanii.

“Sidhani kama kuna haja ya mimi kuharakisha kukimbilia kwenye ndoa, kwanza mashabiki zangu wanatakiwa watambue #Lulu ni 'brand', nina maisha yangu binafsi ya kuyajenga.” ameeleza.

“Wote tunajua ukishaingia kwenye ndoa ni jukumu lingine kubwa sana ambalo nikili harakisha itabidi nijikane mimi kama 'brand', itafika siku tu, #Lulu ataolewa, atakuwa na ndoa,” aliongeza Lulu.

Itakumbukwa, Lulu alishavishwa pete ya uchumba na Francis Ciza maarufu kama #Majizzo, mwishoni mwa Septemba 2018 na siku kadhaa baadaye alitolewa mahari na mchumba wake huyo na kinachosubiriwa hivi sasa ni harusi yao tu.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...