LUC Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa yeye sio mbaguzi ingekuwa hivyo asingeweza kufanya kazi ndani ya bara la Afrika kwa miaka mingi.
Leo, Eymael ametimuliwa kazi na mabosi wake Yanga kutokana na kitendo chake cha kutoa lugha zisizo za kiungwana zenye viashiria vya ubaguzi wa rangi kwa mashabiki wa Yanga kupitia sauti yake kwa vyombo vtya habari.
Kauli aliyoisema Eymael kuhusu mashabiki ni hii hapa:-"Sifurahii nchi hii (Tanzania). Nyinyi ni watu ambao hamjaelimika. Nimechukizwa. Sina gari, WiFi au DSTV. Mashabiki hawajui chochote kuhusu soka. Ni kama nyani au mbwa wanavyopiga kelele."
Kuhusu ubaguzi wa rangi Eymael amesema:"Kama ningekuwa mimi ni mbaguzi wa rangi basi nisingeweza kufanya kazi miaka mingi Afrika, pia nisingeweka ishara ya kupinga ubaguzi na ndio maana jana nilipiga goti moja pale uwanjani,".
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment