Search This Blog

Thursday, July 2, 2020

AU: Corona imesababisha hasara ya dola bilioni 55 barani Afrika


Kkamishna wa Miundombinu na Nishati wa Umoja wa Afrika AU amesema kuwa, nchi za bara hilo zimeshapata hasara ya dola bilioni 55 za ushuru wa usafiri na utalii katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kutokana na ugonjwa hatari wa COVID-19.

Bi Amani Abou-Zeid amewaambia waandishi wa habari kwamba madhara yaliyopatikana na kutokana na hatua zilizochukuliwa za kukabiliana na ugonjwa wa corona, kufungwa mipaka, kuzuiwa safari za anga n.k, ni makubwa sana kwa uchumi wa nchi za Afrika. Amesema, utalii na usafiri husaidia takriban asilimia 10 ya pato la ndani la nchi zote za Afrika.

Amesema, barani Afrika kuna familia milioni 24 ambazo maisha yao yanahusiana moja kwa moja na safari na utalii na kwamba cha kusikitisha zaidi ni kuwa janga la corona limekuja mwaka huu ambapo Afrika ilikuwa inatarajia kushuhudia ongezeko kubwa la safari hasa za anga.


Amesisitiza kuwa, uchumi wa Afrika umepata pigo kubwa na watu wengi wamepoteza ajira. Mashirika ya ndege ya Afrika yamesimamisha kikamilifu shughuli zao ya yamepata hasara ya takriban bilioni nane za ushuru tu katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya kuenea kirusi cha corona bila ya kuhesabu hasara za mashirika hayo katika mali zao kama ndege, majengo, hisa zao n.k.

Bi Amani Abou-Zeid ameongeza kuwa, baadhi ya mashirika makubwa kama lile la Ethiopian Airlines yilionesha nia ya kutumia fursa hiyo kujiimarisha zaidi kupitia kununua hisa za makampuni madogomadogo lakini nayo yameshindwa kutokana na kwamba ugonjwa wa corona umevuruga mpango wa Umoja wa Afrika AU wa kuwa na soko moja tu na usafiri wa anga barani Afrika.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...