Search This Blog

Tuesday, June 16, 2020

Watanzania 249 waliokwama nchini India warejea nyumbani


Zaidi ya abiria 249 wamewasili hapa nchini baada ya kukwama nchini India kwa zaidi ya miezi mitatu kufuatia mlipuko wa virusi vya corona ulioikumba dunia na kusababisha nchi nyingi kufunga safari za kutoka na kuingia katika nchini hizo.

Wakizungumza na Channel Ten katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baadhi ya abiria waliorejea nchini pamoja na ndugu waliokuja kuwalaki wameipongeza na kuishukuru serikali ya Tanzania kwa hatua iliyochukua kuwaandalia ndege kwa ajili ya safari ya kurejea hapa nchini, hatua ambayo wamesema ni kielelezo cha kuwajali wananchi wake.

Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Josephat Kagirwa amesema kwamba shirika hilo limehakikisha safari inafanikiwa na litaendelea kutoa huduma za usafiri ipasavyo ikiwemo ya kuwarejesha abiria walio kwama katika nchi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...