Search This Blog

Tuesday, June 16, 2020

UEFA yatangaza kurudi na mfumo wa mechi 12

Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), linatarajiwa kumaliza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda wa siku 12 jijini Lisbon-Ureno, mwezi Agosti mpango ambao utaamuliwa leo kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya UEFA .

Hatua za robo fainali, nusu fainali na fainali zitachezwa jijini Lisbon kuanzia tarehe 12-23 Agosti huku timu zilizosalia kucheza mechi za marudiano hatua ya 16 bora kama Chelsea na Bayern Munich na Manchester City na Real Madrid kusemekana kuchezwa kwenye Viwanja vyao binafsi.

Mpango huu umependekezwa kwa ajili ya kumaliza mashindano mapema kuliko kucheza kama kawaida nyumbani na ugenini, mfumo huu pia utatumika kumaliza mashindano ya Europa nchini Ujerumani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...