Search This Blog

Friday, June 12, 2020

RAFAEL: Tolisso nenda Man United

MUNICH, UJERUMAN. NDIO ipo hivi, kiungo wa Bayern Munich Corentin Tolisso anatajwa kuwa kwenye harakati za kutimka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu.

Kiungo huyo hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza na sasa ameshauriwa kuondoka na kusaka nafasi ya kujiunga na Manchester United ili kuja kuwa staa mkubwa duniani.

Hata hivyo, Manchester United ya Ole Gunnar Solskjaer kwa sasa inaonekana kuwa na watu wa nguvu kwenye eneo la katikati kutokana na huduma ya Bruno Fernandez aliyetua klabuni hapo Januari, mwaka huu.

Lakini, beki wa zamani wa Manchester United anayekipiga Olympic Lyon kwa sasa, Rafael da Silva amemwambia kiungo huyo mwenye miaka 25, awasiliane na mabosi wa Man United.

Rafael na Tolisso mwenye thamani ya pauni 31 milioni, wamewahi kucheza wote kwa wababe hao wa Ufaransa kabla ya kutimkia Bayern Munich, ambako anasugua benchi kwa sasa.

“Ni mmoja kati ya viungo bora ambao nimewahi kucheza nao, nafikiri Manchester United ndio itakuwa sehemu sahihi kwake, kama atakwenda hapo,” alisema Rafael kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Advertisement

Tolisso alitua Allianz Arena akitokea Lyon mwaka 2017, lakini tangu wakati huo amekuwa mchezaji wa kusubiri benchi kutokana na kuanza kwa majeraha mfululizo.

Mkataba wa kiungo huyo na Bayern Munich unafikia tamati mwaka 2022 na ripoti zinaeleza kwamba, amekuwa fiti kurejea uwanjani.

Tolisso ameshinda Kombe la Dunia mwaka 2018 akiwa na timu ya Taifa ya Ufaransa pamoja na kubeba taji la Bundesliga akiwa na wababe hao wa Ujerumani.

Licha ya awali Man United kuulizia huduma ya Tolisso, lakini kwa sasa nguvu zao ziko kwenye kunasa saini ya winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, anayepatikana kwa pauni 100 milioni. Tayari, mabosi wa Borrusia wameonyesha wasiwasi wa ya kumkosa Sancho, ambaye mara kadhaa ameeleza kwamba moja ya ndoto zake ni kuichezea Man United.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...