Search This Blog

Friday, June 12, 2020

Ubaguzi watibua madili kibao ya Yorke

LONDON, ENGLAND. ISHU ya George Floyd imezidi kuwaibua mastaa wa soka duniani wenye asili ya Afrika, ambao wamefichua matukio mbalimbali ya ubaguzi wa rangi.

Supastaa wa zamani wa Manchester United, Dwight Yorke amefichua kuwa amekuwa kwenye mapambano makali kusaka ajira ya ukocha.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja, Yorke alisema kuwa wachezaji wengi weusi wamekuwa wakikutana na matukio yasiyo ya kawaida kwenye soka ikiwemo kunyimwa fursa za kuonekana na kupata ajira hasa za ukocha.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United na Aston Villa, alifichua kuwa kuna wakati wachezaji weusi wanabaguliwa hata kutoa maoni licha ya kuwa na umuhimu kwenye timu.

Kupitia mahojiano hayo, Yorke alieleza namna kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson, alivyompigania ili kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kuwa kocha.

“Ukweli ni kuwa Ferguson ambaye amekuwa msaada kwangu, kama mzazi, nimekuwa nikisema nilipoomba kazi Aston Villa, nilimfuata na kumueleza nilichokuwa nakitaka,” alisema Yorke.

Advertisement

Alisema baada ya kumueleza mahitaji yake, Ferguson alimpa ushauri kulingana na uzoefu wake, aliyapokea mawazo yake na kuyafanyia kazi, wakati huohuo alimpigia simu na kupokea.

Pia, alisema kuwa Ferguson alimweleza kama atahitaji chochote kutoka kwake na hata ikiwezekana kupata nafasi ya kuwa kocha kwenye vikosi vya Manchester United, basi yupo tayari kumsaidia.

Hata hivyo, Yorke alisema kuwa wachezaji weusi imekuwa shida hata kupata mahojiano na vyombo vya habari na hilo limekuwa tatizo endelevu.

“Ushahidi upo wazi sana, angalia kwa sasa kama utaona kocha mweusi kwenye Ligi Kuu England…makocha wengi weusi wapo na wana uwezo mkubwa lakini, kipaumbele ni kwa watu weupe ambao wengine hawana uwezo wala uzoefu,” alisema staa huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha Man United kilichoshinda mataji matatu kwa mpigo mwa mwaka 1999.

Hata hivyo, Yorke ameahid kuwa atapambana na yote kwa kuwa bado ana matumaini ya kupata nafasi na kufanya vizuri jambo ambalo litasaidia watu weusi kuonekana.

Kauli ya Yorke haina tofauti na ile ya winga wa Manchester City, Raheem Sterling ambaye hivi karibuni alikaririwa akisikitishwa na kitendo cha makocha weusi kushindwa kupewa nafasi licha ya kuwa na uwezo mkubwa kwenye kazi hiyo.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...