Aliyewahi kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Mtakatifu John Paulo wa Pili amekumbukwa leo katika siku ya miaka 100 tangu alipozaliwa, kwa kufanyika misa maalum katika makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican na katika nchi yake ya Poland.
Misa hizo zimefanyika leo kumkumbuka kiongozi huyo wa kidini wa kanisa Katoliki katika wakati ambapo Kanisa hilo nchini Poland linajikuta likikabiliwa na madai mapya ya kuhusika kwa viongozi wa kidini katika vitendo vya unyanyasaji wa kingono.
Sherehe hizo zimefanyika katika mji mdogo wa Wadowice ambako Karol Wojtyla alizaliwa Mei 1920 na pia mjini Warsaw na Vatican ambako waumini wa Kikatoliki walifanya maombi ya shukrani kwa ajili ya mtakatifu John Paulo wa Pili aliyewahi kuwa papa kuanzia mwaka 1978 mpaka mwaka 2005 alipofariki.

No comments:
Post a Comment