Search This Blog

Monday, May 25, 2020

Lyon yakwama kupindua meza

PARIS, UFARANSA. IMETOKA hiyo, ikirudi pancha. Olympique Lyon, Toulouse na Amiens zimegonga mwamba kwenye mpango wao wa kukata rufaa kupinga msimu wa Ligue 1 kumalizwa mapema kabla ya mechi kumalizika baada ya kuambiwa, hakuna kesi.

Tofauti na Ligi Kuu kubwa nyingine za Ulaya, Ligi ya Soka ya Kulipwa huko Ufaransa (LFP) yenyewe ilichukua uamuzi wa kumaliza msimu mapema mwishoni wa Aprili.

Ligi Kuu England ilisimama katikati ya Machi kutokana na janga la corona, lakini LFP ilifikia uamuzi wa kumaliza kabisa msimu wakifuata nyayo za Ligi Kuu Ubelgiji (Pro League) na Uholanzi (Eredivisie) waliomaliza ligi zao kutokana na janga la corona.

Msimamo wa mwisho wakati ligi inasimamishwa ukizingatia pointi zilizobebwa kwa kila mechi, uliifanya Paris Saint-Germain kutangazwa mabingwa huku timu mbili za mkiani, Toulouse na Amiens zilishushwa daraja.

Wakati huo huo, Lyon wao walishika nafasi ya saba kwenye msimamo na hivyo kushindwa kufuzu michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997. Kutokana na hilo, Lyon iliamua kwenda mahakamani pamoja na timu hizo zilizoshuka daraja kupinga uamuzi wa LFP jambo ambalo lilitupwa kando na mahakama hiyo Ijumaa iliyopita.

Rais wa Lyon, Jean-Michel Aulas amekuwa na wasiwasi kwamba kushindwa kufuzu kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao kunaweza kukiweka kikosi chake kwenye hatari kubwa ya kupoteza mastaa wake muhimu ambao watahama mwishoni mwa msimu.

Advertisement

Mchakato huo utafanya pia Ligue 2 msimu ujao kuwa na timu 22 badala ya timu 20 zilizoeleka kabla ya janga la corona.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...