Search This Blog

Monday, May 25, 2020

KAZI IPO..Pochetinho kutua Newcastle silaha za kwanza hizi hapa

NEWCASTLE, ENGLAND. KWANI mmejipangaje huko kwa sababu mambo ni moto mjue? Hii inawahusu wapinzani wa Newcastle United kwenye Ligi Kuu England msimu ujao, ambao lazima wataingiwa kiwewe mapema tu.

Mambo matamu yananzia kwa kocha na Mauricio Pochettino amefungua milango na kusema yupo tayari kufanya kazi kwenye mpango huo madhubuti kabisa wa kuiweka Newcastle United juu ya ramani.

Klabu nyingi vigogo vimekuwa vikipiga hesabu ya kumchukua Muargentina huyo baada ya kufutwa kazi huko Tottenham Hotspur tangu Novemba mwaka jana na timu zilikuwa zikihofia kulipa fidia.

Lakini, sasa kocha huyo yupo huru kujiunga na timu yoyote itakayohitaji saini yake. Tangu hapo, jina lake limekuwa likihusishwa na Newcastle United, ambao si muda mrefu watakuwa chini ya tajiri mwenye pesa ndefu, mwana wa mfalme wa Saudi Arabia, Mohamed bin Salman.

Pochettino alisema: “Siku zote utakuwa na ndoto za kufanya kazi kwenye klabu sahihi, kwenye mipango sahihi. Nipo tayari kwa ajili ya mpango huo mahususi.”

Ujio wa bilionea Bin Salman huko Newcastle unadaiwa kwamba, utaifanya timu hiyo kuwa na pesa ndefu kwenye usajili kutokana na kuwapo na mpango matata wa kuanzisha uwekezaji kwenye klabu hiyo kwa kuanzia katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Advertisement

Pochettino, anayetajwatajwa huko St James’ Park, tayari ameanza kuwatia watu ubaridi baada ya kutaja wachezaji wake bora waliopo kwenye Ligi Kuu England na kuibua wasiwasi, huenda akaanza nao atakapobeba mikoba rasmi ya kukinoa kikosi cha Newcastle United?

Kwenye orodha hiyo, Pochettino hakuwataja kabisa mastaa wake wa zamani aliowanoa Spurs, akiwamo Harry Kane na Son Heung-min – huku vichwa vyake vitatu ni Kevin De Bruyne, Sergio Aguero na Roberto Firmino.

De Bruyne anatajwa kama mmoja wa viungo bora kabisa duniani kwa sasa, akiongoza kwenye Ligi Kuu England kwa kupiga asisti 16 msimu huu, nne zaidi ya mchezaji anayemfuatia kwenye ubora huo wa kupika pasi za mabao kwenye mikikimikiki hiyo.

Kuhusu Aguero, ambaye ni chaguo lake la pili Pochettino, straika huyo Muargentina ameendelea kuonyesha kwamba, yeye ni moto kwenye kupasia nyavu, akifunga mara 23 katika mechi 30 alizocheza msimu huu. Mastaa hao wawili walikuwa muhimu wakati Manchester City ilipobeba ubingwa wa Ligi Kuu England kwa misimu miwili mfululizo miaka miwili iliyopita, ikiwamo msimu ambao timu yao ilifikisha pointi 100, msimu wa 2017/18.

Wakati Aguero na De Bruyne wakionekana kwamba wangekuwa chaguo la mashabiki wengi pia, Pochettino mchezaji wake watatu amewaacha wengi bila ya kumfikiria, akimtaja Mbrazili, Firmino.

Alipoulizwa awataje majina, Pochettino alisema: “(Kevin) De Bruyne, moja. (Sergio) Aguero mbili. Mwingine? Sijui nini niwaambie, lakini ni Roberto Firmino. Wapo wachezaji wengine wengi tu.”

Pochettino amemtaja Firmino kwa sababu amekuwa msaada mkubwa kwa wachezaji wanaomzunguka na kuwapa uhuru wa kutosha wa kufunga mabao.

Kwenye kikosi cha Liverpool, mastaa Sadio Mane na Mohamed Salah, wamekuwa wakifunga kiasi cha kugawana tuzo ya Kiatu cha Dhahabu kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini mhusika mkuu wa mabao yao ni Firmino.

Msimu huu, Mane amefunga mabao 16, Mo Salah mabao 20, wakati Firmino amefunga 11, lakini akiwa muhimu kwenye kuwatengenezea mabao wenzake, akiwa na asisti 10, akishika namba mbili kwa wapishi wa mabao kwenye kikosi hicho cha Jurgen Klopp, ambacho msimu huu kimebakiza pointi chake tu kubeba ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya kusubiri wa miaka 30.

Hayo ndio machaguo ya Pochettino na haieleweki kama ataanza mchakamchaka wa kunasa saini zao kama atapewa mikoba ya kuinoa Newcastle United wakati itakapobebwa rasmi na bilionea Bin Salman.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...