Search This Blog

Monday, May 25, 2020

Kompany anachowaambia Liverpool? Utacheka

LONDON ENGLAND. STAA wa zamani wa Manchester City, Vincent Kompany amesema anawaonea huruma sana Liverpool na kisha kuwapiga kijembe: “Hivi nyie watu mna bahati mbaya kiasi gani!”

Nahodha huyo wa zamani wa Man City, Kompany amebeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne katika kipindi chake alichokuwa na miamba hiyo ya Etihad na anadhani kwamba Liverpool bado hawana uhakika wa kubeba taji hilo licha ya kubakiza pointi chache sana msimu huu.

Liverpool inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 25, hivyo inahitaji pointi tano tu kubeba ubingwa, lakini janga la virusi vya corona limekuja kutibua mambo na sasa limekuwa suala la simtofahamu juu ya kuendelea kwa ligi hiyo ili kumalizia mechi zilizobaki.

Kompany alisema: “Najaribu kuvuta picha, kisha nawaonea huruma Liverpool, wana bahati mbaya kiasi gani. Lakini, ndiyo hivyo, tuwe na matumaini tu kama ni ushindi basi watapata inavyostahili.”

Mpango uliopo kwa sasa ni ligi kurejea na kuanzia Juni 12, lakini kumekuwa na mambo mengi yenye utata hata kwenye suala la kuwakabidhi kocha Liverpool kama jambo hilo litafanyika mbele ya mashabiki au la.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu England, Richard Masters amekiri kwamba bado kuna wasiwasi mkubwa kama Liverpool itakabidhiwa taji lao mbele ya mashabiki watakapolibeba na jambo hilo litafanyika kama tu kutakuwa na usalama wa kutosha kuhusu afya za watu katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Advertisement

Kompany alifunga bao muhimu zaidi msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Leicester City na hivyo kupata pointi zilizoifanya Man City kubeba ubingwa wa kuipiku Liverpool. Mwishoni mwa msimu aliondoka Man City baada ya kuichezea kwa miaka 11 na kwenda kujiunga na timu yake ya zamani ya Anderlecht ya Ubelgiji.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...