Search This Blog

Wednesday, May 20, 2020

Kimbunga Amphan chaikumba India


Kimbunga kikubwa ambacho hakijatokea miongo kadhaa iliyopita cha Amphan, kimeipiga India upande wa mashariki leo jumatano, kikiwa na upepo unaotembea hadi kilometa 190 kwa saa.

Mkurugenzi wa hali ya hewa nchini India Sanjib Banerjee amesema kimbuga hicho kimeipiga kisiwa cha Sagar kilichopo katika pwani ya India.

Afisa huyo wa hali ya hewa amesema kimbunga kinaweza kusababisha madhara zaidi India na Bangladesh, ambapo wakazi milioni kadhaa katika eneo la Pwani wameondolewa kukimbia kimbunga hicho.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...