Search This Blog
Wednesday, May 20, 2020
BOXER, nyota wa YANGA afichua maana ya jina lake
PAUL Godfrey maarufu kama Boxer beki wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kupewa jina hilo ni spidi yake ya kukimbiza upepo ndani ya uwanja.
Boxer alifanya vema msimu wa 2018/19 chini ya Kocha Mkuu winyi Zahera na alimuweka benchi mkongwe Juma Abdul ambaye kwa sasa amerejea kwenye ubora wake.
Akizungumza Boxer amesema kuwa awali wengi walikuwa wanamuita Paul ila kutokana na spidi yake ndani ya uwanja ikabadili upepo wa jina lake.
“Nilikuwa ninaitwa Paul na wenzagu ila kutokana na spidi yangu ya kukimbia ndani ya uwanja ilinifanya nibadilishwe jina na kuitwa Boxer ambalo ni jina la pikipiki.
“Boxer inaaminika kuwa na spidi kubwa ndani ya uwanja sasa hapo wachezaji wenzagu wakawa wananifananisha na bodaboda hiyo,” amesema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment