Search This Blog

Thursday, May 21, 2020

Diwani kortini kwa kupokea rushwa ya sh mil.1/



Diwani wa Kijichi katika Manispaa ya Temeke kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elias Mtarawanje (29), amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo kushawishi na kupokea rushwa ya Sh. milioni moja kutoka kwa Yusuf Omary.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake jana katika mahakama ya Wilaya ya Temeke iliyoketi chini ya hakimu mkazi, Ctherine Madili.

Mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mwanakombo Rajabu , alidai kuwa, Februari 6 mwaka huu , Mtoni Kijichi ,Wilaya ya Temeke , Jijini Dar es salaam mshtakiwa akiwa Diwani wa kata ya Kijichi aliomba rushwa ya sh. milioni moja kutoka kwa Omary  kama kishawishi kwake ili asiweze kulipa malipo ya fidia ya eneo jambo ambalo amelifanya tofauti  na uhusiano na shughuli za muajiri wake.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...