Imeripotiwa kuwa wale ambao walikwenda Ujerumani kwa sababu za kibiashara au za kitalii lakini muda wa visa zao umemalizika,basi hawatochukuliwa hatua yoyote kutokana na hatua mpya zilizowekwa kupambana na janga la dunia nzima la virusi vya Corona.
Katika taarifa iliyoandikwa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, imeelezwa kuwa hakuna adhabu yoyote itakayotolewa kwa wale waliokuwa na viza za kufanya kazi na za kitalii na muda wa viza hizo umekwisha.Badala yake wapo huru kuendelea na shughuli zao bila kuwa na viza mpaka hapo tarehe 30 Juni.
Imesisitizwa kuwa wale wafanyakazi ambao viza zao za kazi zimeisha muda wanaweza kuendelea kufanya kazi hadi hapo 30 Juni.
Taarifa hiyo imeongeza kwa kusema kuwa hali itatizamwa tena ifikapo tarehe 30 mwezi Juni.

No comments:
Post a Comment