Uturuki yatuma msaada wa madawa na vifaa vya matibabu nchini Uingereza katika juhudi za kupambana na virusi vya corona.
Uturuki yafahamisha kutuma msaada wa madawa na vifaa vyamatibabu nchini Uingereza katika uhudi za kupambana na virusi vya corona, virusi ambavyo tayari vimesababisha maafa makubwa ulimwenguni.
Ndege ya mizigo ya jeshi imeondoka mapema Ijumaa katika uwanja wa ndege mjini Ankara kuelekea nchini Uingereza.
Msaada huo ni pamoja na barakoa aina ya N95 na vifaa vingine ambavyo hutumiwa katika kuzuia maambukizi ya Covid-19.
Wizara ya afya ya Uturuki imesema kuwa kuwa vifaa hivyo ni kwa ajili ya ushirikiano katika kupambana dhidi ya virusi vya corona.
Ndege hiyo aina ya A400M anasubiriwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini London.
Katika mikoba ya vifaa hivyo kumechapishwa beti za shairi şa Mevlana Jalal ad Din Rumi zisemazo : « kuna matumaini hata kama watu wamepoteza matumaini".
Uturuki imetuma pia msaada wa madawa na vifaa vya matibabu nchini Italia, Uhispania, Mekedonia Kaskazini, Montenegro, Serbia, Boznia na Kosovo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment