Search This Blog

Saturday, April 11, 2020

Man United na Shanghai zote zinajifikiria kuhusu Ighalo

Staa wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Shanghai ya China ila kwasasa akiwa kwa mkopo Man United Odion  Jude Ighalo amekanusha vikali taarifa za kuwa amepewa ofa na Man United na Shanghai na kusema kuwa hadi sasa hana ofa.

”Sina ofa nimetulia na nitafanya maamuzi na sitayumbishwa na chochote watu wanachosema, nilikuja Man United na nikakubali kukatwa mshahara ili nicheze kwa sababu nilitaka” -  Ighalo

”Chochote kinaweza kutokea mwisho wa msimu, kwanza nataka msimu uishe na mkopo wangu uishe halafu nitajua nini kitatokea baada ya hapo” - Ighalo

Jude Odion Ighalo amekuwa na mkopo mzuri ndani ya Man United toka alipowasili dirisha dogo la January 2020, Ighalo hadi michezo inasimamishwa sababu ya mlipuko wa virusi vya Corona alikuwa kaitumikia Man United katika game 8, magoli manne na kota assist moja, kitu ambacho kimewashangaza wengi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...