Umoja wa Ulaya katika juhudi za kupambana na virusi vya corona umefahamisha kwamba utatoa msaada wa Euro milioni 80 kwa Sudani kwa ajili ya kuzuia na kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Msaada huo utatolewa kwa lengo la kuhakikisha kwamba idara ya afya nchini humo haisumbuki katika juhudi zake dhidi ya virusi vya corona.
Jarida rasmi la Sudani limefahamishakuwa Abdullah Hamduk amezungumza kwa njia ya simu na kamishana wa masuala ya ushirikiano wa kimataifa Umoja wa Ulaya Jutta Urpilainen.
Imefahamishwa kuwa katika mazungumzo yao hao, kamishna huyo wa Ulaya amesema kuwa Umoja wa Ulaya utatoa kiwango cha Euro milioni 80 kwa Sudani kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya corona.
Waziri wa afya wa Sudani Ekrem ali et Tum alifahamisha kuwa wizara yake inahitaji kiwango cha dola milioni 120 ili kukabiliana na virusi vya corona.
Watu wanne wamekwishafariki kwa virusi vya corona nchini Sudani hum-ku watu wengine 29 wakiripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

No comments:
Post a Comment