Search This Blog

Tuesday, April 14, 2020

Marekani kusitisha ufadhili wa WHO kukabiliana na corona

Rais wa Marekani , Donald Trump amesema kuwa uongozi wake utasitisha ufadhili kwa Shirika la afya duniani (WHO).

Amesema WHO imeshindwa kufanya majukumu yake muhimu katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

Ameishutumu Umoja wa mataifa kwa kutoweza kukabiliana na kusambaa kwa janga hili la virusi vya corona ambavyo vilianzia nchini China, na linapaswa kulaumiwa.

Aidha rais Trump mwenyewe alikosolewa nchini mwake kwa namna anavyokabiliana na mlipuko huo nchini mwake.

"Ninawapa muongozo utawala wangu kusitisha ufadhili wakati Shirika la afya duniani likiwa linachunguzwa katika majukumu yake yaliyoshindwa kuyatimiza katika kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona ," Bwana Trump aliwaambia waandishi katika White House.

Shirika la afya duniani -WHO limeshindwa majukumu yake muhimu na wanapaswa kuwajibishwa, " aliongeza.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres alisema kuwa wakati huu si wakati wa kukata ufadhili kwa WHO.

Marekani ndio mfadhili mkubwa wa WHO' anayetoa ufadhili wa kiasi cha dola milioni 400 ambayo ni 15% ya bajeti yake ya mwaka jana.

China ilichangia mwaka 2018-19 karibu dola milioni 76m na yapata dola milioni 10 katika ufadhili, kwa mujibu wa mtandao wa shirika la afya duniani.

Shirika hilo lilitenga kiasi cha dola milioni 675 kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na limeripotiwa kuwa litaongeza fedha hizo hadi karibu dola bilioni moja.

"Mlipuko huu wa ugonjwa wa ovid-19 unatia wasiwasi kama ukarimu wa Marekani umepewa kipaumbele sahihi au la," rais alisema.

Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona duniani kwa kuwa na wagonjwa 608,377 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo kufikia 25,981.

Rais Trump ameishutumu WHO kwa kushindwa kukabiliana na mlipuko huu ulipoanza kwa mara ya kwanza mjini wa Wuhan.

"Hivi WHO imefanya kazi yake ipasavyo kwa kutumia wataalamu wake wa afya kuchunguza hali ilivyo China na kubaini ukosefu wa uwazi kwa kuwa kuna idadi ndogo ya vifo vilivyotokana na mlipuko huo," aliwaambia waandishi.

"Tukibaini hayo tutaweza kuokoa maisha ya maelfu ya watu na kuzuia uchumi wa dunia kuanguka. Lakini WHO iko tayari kuiamini China bila kuangalia uhalisia na kutetea hatua zinazochukuliwa na serikai ya China.

Ripota wa White House walinukuu kuwa bwana Trump mwenyewe alisifu itihada za China katika kukabilianna na janga hili na kuhofia hatari ya ugonjwa huo nchini mwake.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...